SIKU WANAWAKE DUNIANI
Wanawake wa RUCU mmeendelea kuonesha mfano bora wa uongozi, mshikamano na kujituma. Katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08/03/2026, mmeendelea kukiheshimisha na kukitangaza Chuo chetu kwa nguvu, fahari na umoja.
Kupitia mchango wenu mkubwa katika taaluma, malezi na maendeleo ya jamii ya chuo, mmeendelea kuthibitisha kuwa RUCU ni mahali salama na bora kwa kujifunza na kukuza vipaji vya vijana wetu.
Kwa wazazi, walezi na wadau wote wa elimu, RUCU inaendelea kuwa mazingira yenye maadili, usalama na malezi bora kwa wanafunzi wenu. Tunawakaribisha kuendelea kuiamini RUCU kama sehemu sahihi ya kuwajenga watoto wenu kitaaluma na kimaadili.
Source: RUCU