Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) kinaendelea na maandalizi ya Mahafali ya 19, yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa, tarehe 27 Novemba 2026, katika Viwanja vya RUCU, Iringa, kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Katika kuhakikisha mahafali hayo yanafanyika kwa mafanikio, Chuo kinawakumbusha wahitimu wote wa mwaka wa masomo 2025/2026 kukamilisha taratibu muhimu kwa wakati.

Maelekezo Muhimu kwa Wahitimu
1. Wahitimu wote wanatakiwa kuzingatia yafuatayo:
2. Kukamilisha Clearance: Wahitimu wanatakiwa kukamilisha taratibu za Clearance kupitia mfumo wa SIMS.
3. Malipo ya Joho: Kila mhitimu anatakiwa kulipia TSh 40,000/= kupitia Control Number inayopatikana kwenye mfumo wa SIMS.
4. Kuchukua Majoho: Majoho yatatolewa kuanzia tarehe 16 hadi 25 Novemba 2026.
5. Convocation na Mazoezi ya Mahafali: Wahitimu wote wanatakiwa kuhudhuria shughuli hizi Alhamisi, tarehe 26 Novemba 2026, kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Chuo kinawapongeza wahitimu wote kwa hatua muhimu waliyofikia katika safari yao ya kitaaluma. Aidha, kinawakaribisha wazazi, walezi, familia, marafiki na wadau mbalimbali kushiriki katika kusherehekea mafanikio haya.
Wahitimu wanahimizwa kukamilisha maandalizi yote kwa wakati ili kuhakikisha ushiriki wao katika Mahafali ya 19 unafanyika kwa utaratibu na ufanisi.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Chuo kupitia 0699 997 950

TUKUTANE RUCU! TUKUTANE IRINGA!
Share:

Related articles

Chat with us