MAHAFALI YA 19 - RUCU
Mgeni Maalum katika mahafali hayo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James, alisema Serikali ya Mkoa inathamini mchango wa RUCU na akahimiza ushirikiano wa karibu kati ya chuo, taasisi za Serikali na sekta binafsi katika utafiti, ubunifu na huduma kwa jamii. Alisisitiza kuwa tafiti zinazofanyika vyuoni zisibaki maktabani, bali zibadilishe maisha ya wananchi.
Akizungumza na wahitimu, Mhe. James aliwataka wasisubiri kuajiriwa pekee, bali wajiajiri, waanzishe biashara na watengeneze ajira kwa wengine. "Msiwe kizazi kinachosubiri fursa; kuweni kizazi kinachozibuni," alisema.
Tazama picha za Mahafali ya 19 ya RUCU hapa:
PICHA ZA MAHAFALI-1
PICHA ZA MAHAFALI-2